Kufanya bajeti (au mpango wa pesa) hukuwezesha kuweza kuona pesa zinazoingia na kutoka kaya yako. Inakusaidia kudhibiti pesa zako na kuweka akiba kwa vitu unavyohitaji.
Jinsi bajeti inavyofanya kazi
'Bajeti' ni mpango wa pesa unaokuonyesha pesa zinazoingia na kutoka kaya yako. Hii inaweza kuwa kila wiki, wiki mbili au mwezi.
Mpango wako wa pesa hukusaidia kujua ni kitu gani cha muhimu zaidi. Kisha unaweza kuchagua kupunguza mambo ambayo huhitaji na uhifadhi zaidi kwa mambo unayohitaji.
Fanya bajeti yako
Fuata hatua hizi ili kuanza.
Ili kurahisisha, pata usimamizi rahisi wa pesa ili kukusaidia kuhesabu kwa ajili yako.
1. Orodhesha pesa zinazoingia
Orodhesha pesa zinazoingia katika kaya yako ('mapato'), kama vile:
- mshahara kutokana na kazi yako
- malipo ya pensheni au pesa kutoka Centrelink
Ili kupata maelezo haya, angalia hati zako za malipo, taarifa za benki mtandaoni au taarifa za benki.
2. Orodhesha pesa zinazotoka
Orodhesha pesa zinazotoka ('gharama'), kama vile gharama za maisha, bili na malipo ya deni:
- matumizi ya vitu vya msingi ya kila wiki kama vile chakula, mboga mboga, usafiri
- bili za kawaida kama vile kodi au rehani, umeme, simu, ulipaji wa mkopo, bima
- matumizi madogo ya mara kwa mara kama vile mavazi, ada za shule, usajili wa gari, gharama za matibabu
Angalia taarifa zako za benki mtandaoni au, bili na taarifa za kadi ya mkopo. Zingatia gharama ni ya nini, ni kiasi gani na wakati unapolipa.
3. Linganisha pesa kuingia na pesa kutoka
Linganisha orodha yako ya pesa zinazoingia na kutoka.
Ikiwa una pesa zaidi zinatoka kuliko kuingia - ni wakati wa kufanya chaguo fulani. Fikiria ni nini:
- 'mahitaji' (huwezi kuishi bila kuwa nayo)
- 'matakwa' (unaweza kuishi bila kuwa nayo, angalau kwa muda)
Amua unachoweza kukata au kupunguza. Kuwa wa kweli - usifanye iwe ngumu sana kushikamana nayo.
Unapopunguza, toa pesa zinazotoka kutoka kwa pesa zinazoingia.
Kiasi kilichobaki ni kiasi gani unaweza kuweka kwenye lengo lako la kuweka akiba.
4. Weka lengo lako la kuweka akiba
Kuweka lengo la kuweka akiba kunakufanya kunahisi vizuri na hukusaidia kuwa makini.
Haijalishi lengo lako ni kubwa au dogo kiasi gani, anza tu. Kuweka kando hata kiasi kidogo mara kwa mara huongezeka juu ya muda.
Fanya bajeti yako iendane na wewe
Tenganisha matumizi yako na kuweka akiba
Jaribu kuanzisha akaunti tofauti za benki kwa:
- matumizi ya kila siku na bili
- akiba
Ukiweza, panga uhamishaji wa mara kwa mara wa baadhi ya malipo yako kwenye akaunti yako ya akiba siku ya malipo. Kwa njia hii, unahifadhi bila kufikiria juu yake.
Uliza mwajiri wako, rafiki au mwanafamilia ikiwa unahitaji usaidizi ili kufanya hivyo.
Lipa bili zako kwa kiasi kidogo
Wasiliana na watoa huduma wako, kama vile umeme na gesi, ili kuuliza kuhusu kulipa bili kwa kiasi kidogo ('instalments').
Unaweza kulipa kwa wiki mbili au kila mwezi, ili kuepuka mshtuko wa bili kubwa.
Ukipata malipo ya Centrelink, unaweza kutumia huduma yao ya Centrepay bila malipo kwa kufanya hivyo.
Pata usaidizi ikiwa unahitaji
Kuna msaada wa bure unaopatikana, ikiwa unahitaji:
- Kwa usaidizi katika lugha yako, pigia simu kwa huduma ya utafsiri na ukalimani TIS National kwa 131 450. Watapata mkalimani wa kupigia simu huduma unayohitaji usaidizi nayo.
- Kwa usaidizi wa kutatua masuala ya pesa, piga simu bila malipo Nambari ya Msaada ya Deni la Taifa kwa 1800 007 007. Nambari hii ya msaada inafunguliwa Jumatatu hadi Ijumaa, saa 3.30 asubuhi (9:30am) hadi 10.30 jioni (4:30pm).