Jua jinsi ya kufuatilia matumizi yako na kulipa bili zako kwa wakati. Hii husaidia kupunguza mkazo au ugumu wa pesa, kwa hivyo hauishi kutegemea kila ukilipwa mshahara tu.
Bili na jinsi ya kuzilipa
'Bili' ni kile unacholipa kwa bidhaa au huduma unayopata. Utapata bili ya huduma za nyumbani kwako kama simu yako, mtandao, maji, umeme na gesi.
Utatumiwa bili kwa kila huduma unayotumia, kwa kawaida kila mwezi au kila baada ya miezi 3 kulingana na aina ya bili.
Kuna taarifa gani kwenye bili
Bili yako itakuonyesha:
- jumla ya kiasi cha kulipa
- tarehe ya kulipa kwa ('tarehe ya mwisho')
- kiasi cha huduma uliyotumia (kwa mfano, kwa bili ya simu hii itakuwa nambari ya simu ulizopiga)
- njia tofauti za kulipia bili yako
Jinsi ya kulipa bili
Bili yako itakuambia jinsi unavyoweza kulipa, kama vile:
- kupitia benki ya mtandaoni (kwa njia ya kukatwa moja kwa moja au BPAY)
- kwa njia ya simu
- kwa njia ya kadi ya mkopo
- kwenye ofisi ya posta
Dhibiti bili zako
Lipa kwa tarehe ya kukamilisha
Unapopata bili au taarifa ya mkopo, tafuta 'tarehe ya mwisho ya kulipia'. Huu ndio wakati bili, mkopo au urejeshaji wa mkopo unastahili kulipwa.
Unaweza kutozwa ada na mtoa huduma ikiwa utalipia bili kwa kuchelewa.
Kulipa kwa kuchelewa kunaweza pia kuathiri 'alama yako ya mkopo' au 'ukadiriaji wa mkopo'. Hivi ndivyo benki hutumia kuamua kukupa mkopo au kukuruhusu kukopa pesa.
Kwa hivyo ni bora kulipa kwa au kabla ya tarehe ya mwisho ya kulipia.
Lipa bili zako kwa kiasi kidogo
Utagundua kuwa miezi kadhaa una bili nyingi kuliko mingine.
Ili kudhibiti hili, wasiliana na watoa huduma wako, kama vile umeme na gesi, ili kuuliza kuhusu kulipa bili kwa kiasi kidogo ('instalments').
Angalia ikiwa unaweza kulipa kila wiki mbili au kila mwezi, ili kuepuka mshtuko wa bili kubwa.
Ukipata malipo ya Centrelink, unaweza kutumia huduma ya bila malipo ya Centrepay ili kufanya hivyo.
Weka akiba yako sehemu tofauti
Jaribu kuanzisha akaunti tofauti za benki kwa:
- matumizi ya kila siku na bili
- akiba
Ukiweza, panga uhamishaji wa mara kwa mara wa baadhi ya malipo yako kwenye akaunti yako ya akiba siku ya malipo. Kwa njia hii, unahifadhi bila kufikiria juu yake.
Pesa unazohifadhi zinaweza kuwa 'mfuko wa dharura'. Hii hukusaidia kulipia bili kubwa zisizotarajiwa, au kukutunza wewe au familia yako ikiwa jambo fulani litatokea.
Uliza mwajiri wako, rafiki au mwanafamilia ikiwa unahitaji usaidizi ili kufanya hivyo.
Fuatilia matumizi yako
Kujua pesa zako huenda kunaweza kukusaidia kutumia kidogo na kuhifadhi zaidi.
Ili kujua pesa zako zinakwenda wapi siku hadi siku, jaribu kuandika 'shajara ya matumizi'.
Andika kila kitu unachotumia kwa kipindi kimoja cha malipo au angalau wiki. Hii itachukua dakika chache tu kwa siku.
Sio juu ya kujihukumu, ni juu ya kujua tabia zako za kila siku za pesa.
Unaweza kufanya hivyo peke yako, au pamoja na rafiki, mpenzi au familia yako.
Pata usaidizi ikiwa unahitaji
Kuna msaada wa bure unaopatikana, ikiwa unahitaji:
- Kwa usaidizi katika lugha yako, pigia simu kwa huduma ya utafsiri na ukalimani TIS National kwa 131 450. Watapata mkalimani wa kupigia simu huduma unayohitaji usaidizi nayo.
- Kwa usaidizi wa kutatua masuala ya pesa, piga simu bila malipo Nambari ya Msaada ya Deni la Taifa kwa 1800 007 007. Nambari hii ya msaada inafunguliwa Jumatatu hadi Ijumaa, saa 3.30 asubuhi (9:30am) hadi 10.30 jioni (4:30pm).