Bima ni wavu wa usalama kwa mambo yanapokwenda vibaya. Pesa kutoka kwa bima zinaweza kusaidia kulipia gharama ya matengenezo, matibabu, mabadiliko ya usafiri au wizi.
Jinsi bima inavyofanya kazi
Unaponunua bima, unaomba ulinzi dhidi ya hatari ya kutokea kitu kibaya.
Kwa mfano, unaweza kuchukua bima ya nyumba yako na gari lako. Kulingana na sera yako ya bima, 'bima' (kampuni ya bima) itakulipa pesa ikiwa kitu kitaenda vibaya. Kama vile nyumba yako imeharibiwa na dhoruba, au ukipata ajali ya gari. Unapokopa ili kufanya ununuzi mkubwa, kama vile nyumba au gari, kupata bima inaweza kuwa sharti la mkopo wako.
Kabla ya kukupa bima, bima itatathmini kiwango cha hatari yako. Wanaweza kuangalia ikiwa umekuwa na madai ya bima ya awali au ajali, au ugonjwa uliopo.
Unaweza kutathminiwa kuwa hatari zaidi ikiwa hali yako inamaanisha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kwenda vibaya. Kwa mfano, ikiwa unaishi katika eneo la mafuriko (kwa bima ya nyumbani). Au unasafiri kwa nchi yenye kiwango cha juu cha uhalifu (kwa bima ya usafiri). Au unafanya kazi katika hatari kubwa (kwa bima ya maisha).
Masharti ya bima
- Sera ya bima - Makubaliano ya kisheria kati yako na bima ambayo yanakuambia unalipwa nini.
- Malipo ya bima - Unacholipa kwa bima yako, kila mwezi au mwaka. Ikiwa hatari yako ni kubwa, unaweza kulazimika kulipa malipo ya juu zaidi.
- Kiasi cha ziada kwa bima - Kiasi gani unahitaji kulipa kwanza, kabla ya kupata pesa kutoka kwa bima yako.
Aina za bima
Aina tofauti za bima hugharimia kwa mambo tofauti. Hapa kuna aina za kawaida za bima:
- Bima ya gari- kulipia gari lako ikiwa limeharibika au kuibiwa
- Bima ya nyumba (bima ya jengo) - kulipa ili kujenga upya ikiwa kitu kitatokea, kama mafuriko au moto
- Bima ya vitu vilivyomo nyumbani- kulipia vitu vya nyumbani kwako vikiharibika au kuibiwa, kama vile samani za ndani, vifaa au vito
- Bima ya afya - kulipa sehemu ya gharama za matibabu ikiwa wewe ni mgonjwa au umejeruhiwa
- Bima ya maisha - kulipa kiasi fulani cha pesa unapokufa, kwa watu unaowateua katika sera yako
- Bima ya ulinzi wa mapato - kulipa baadhi ya mapato yako ikiwa huwezi kufanya kazi kwa sababu ya ugonjwa au majeraha
- Bima ya mnyama mpenzi- kulipa bili za daktari wa mifugo kwa mnyama wako ikiwa anaugua au kuumia
- Bima ya kusafiri- kulipia ajali, ugonjwa au kuchelewa wakati wa kusafiri
- Bima ya mazishi - kulipia gharama ya mazishi yako unapofariki
Jinsi ya kuchagua bima
Kabla ya kupata bima, angalia ikiwa unaihitaji na unaweza kuimudu. Huenda usihitaji aina fulani za bima, kwa hiyo fikiria kile ambacho kinafaa kwako.
Wakati wa kuchagua bima, linganisha bima katika bima mbalimbali. Angalia:
- malipo ya bima - utalipa nini kila mwezi au mwaka
- kikomo cha malipo - ni kiasi gani unaweza kudai kwa bidhaa au matukio fulani
- pesa ya ziada ya sera - ni kiasi gani unachohitaji kulipa kabla ya kupata pesa kwa dai la bima
- kutengwa - ni vitu au matukio gani ambayo hayatalipwa
- malipo - ikiwa unaweza kulipa kila mwezi (bila gharama ya ziada)
Jinsi ya kudai kwenye bima yako
Ili kufanya madai kwenye bima yako, wasiliana na bima uliyenunua sera kutoka kwake.
Toa maelezo ya dai lako
Eleza kilichotokea, kama vile:
- ajali au tukio - eneo, nini kilitokea, ripoti husika
- unachotaka kudai - ukarabati, gharama za matibabu, kujenga upya, mbadala, mapato yaliyopotea
Inachukua muda gani
Dai la bima linaweza kuchukua miezi. Au miaka, kulingana na aina ya bima.
Ikiwa unahitaji usaidizi wa haraka wa pesa wakati dai lako linatathminiwa, wasiliana na bima yako.
Pata usaidizi ikiwa unahitaji
Kuna msaada wa bure unaopatikana, ikiwa unahitaji:
- Kwa usaidizi katika lugha yako, pigia simu kwa huduma ya utafsiri na ukalimani TIS National kwa 131 450. Watapata mkalimani wa kupigia simu huduma unayohitaji usaidizi nayo.
- Kwa usaidizi wa kutatua masuala ya pesa, piga simu bila malipo Nambari ya Msaada ya Deni la Taifa kwa 1800 007 007. Nambari hii ya msaada inafunguliwa Jumatatu hadi Ijumaa, saa 3.30 asubuhi (9:30am) hadi 10.30 jioni (4:30pm).